Thank you, Alex and Muting'u! This is certainly a first for NCUC and I hope it will help us to reach many more people in East Africa. Thanks for your work to make that happen! Best, Robin On Sep 15, 2009, at 12:05 PM, Alex Gakuru wrote: > Hi Robin, all, > > Grace Muting'u has kindly translated the document into Kiswahili > (spoken by at least 120 million people in East African Community > member countries alone). > > Asante (Thanks) Grace. > > Regards, > > Alex > > ---begins---- > “Porojo Kumi maarufu zaidi kuhusu uhusikaji wa mashirika ya shirika > la ICANN”, na NCUC > > 21 Agosti 2009 > ______________________________________________________________________ > _______ > Porojo ya Kwanza > > “Masirika ya kijamii hayatahusika kwenya ICANN chini ya mpango > uliopendekezwa na NCUC.” > > Uwongo: Wafanyakazi wa ICANN na wengine wanadai kwamba > mashirika ya kijamii hukatwa tamaa yasijihusishe na ICANN > kwa vile mpango uliopendekezwa na ICANN hauhakikishi kwamba > viti katika Kamati ya GNSO vitagawiwa maeneo au washikadau wote. > > Ukweli wa mambo ni kwamba uanachama wa NCUC unawakilisha > mashirika 143 yasiyo ya kibiashara pamoja na watu binafsi. Tangu > mwaka 2008 uanachama wa NCUC umeongezeka kwa zaidi ya 215% > - hii ni kwa mujibu wa mwito wa mashirika ya kijamii. Hakuna shirika > hata moja lisilo la kibiashara lililotoa maoni kwamba kuwepo tu kwa > viti vya maeneo katika Kamati ya GNSO ndipo kungewafanya kushiriki > kwenye ICANN. Katika mashirika yaliyotoa maoni yao, hakuna > lilisosema ya kwamba lingeshiriki kwenye ICANN sharti katiba ya > NSCG ingewahakikishia kiti kwenye Kamati ya GNSO. > > Porojo ya Pili > > “Wengi zaidi kutoka mashirika ya kijamii watashiriki kwenye ICANN > Bodi itakapoingilia” > > Picha ya kweli: Kulazimisha kwa Bodi kwa katiba yake au kutosikiliza > kwa Bodi kwa vikundi vya mashirika ya kijamii kutaonekana kama > kukataliwa kwa maoni ya vile vikundi vingi vilivyoonelea kwamba ni hii > ni dhuluma dhidi ya mashirika ya kijamii. Sifa ya ICANN kati ya > mashirika yasiyo ya kibiashara itaharibika kabisa hatua mwafaka > isipochukuliwa au suluhu kupatikana. Hata kama vitendo hivyo > vingekubalika, matokeo kamili kwa wafanya kazi na kwa katiba > ya NCSG itakuwa kuvinyima nguvu vikundi visivyo vya kibiashara > na kuvifanya hata visipende kushiriki. Kuteuliwa kwa waakilishi na > Bodi hufurutisha vikundi visivyo vya kibiashara na watu binafsi. > Isitoshe, SIC inayowakilisha maeneo au washika dau wote inahitaji > fedha nyingi sana ambayo mashirika mengi yasiyo ya kibiashara > hayawezi kusimamilia. Pia, mpangilio huo utaleta mgawanyiko kati > ya vikundi huku vikipigania wanachama na kura. Vikundi vingi visivyo > vya kibiashara havitaweza kuingia ICANN GNSO chini ya mpango huo. > > Porojo ya Tatu > > Kuwepo kwa upinzani kunaweza kupuuzwa tu kama “kampeni ya > uandikaji barua” > > Hii ni shutma isiyo ya kweli: Upinzani mkali wa mashirika ya kijamii > kwa katiba ya SIC ulitokea si mara moja bali mara mbili. Pia, kulikuwa > na ongezeko kubwa la wanachama wa NCUC lililotokana na kutopendezwa > kwa jamii yote kwa jumla na vitendo vya wafanyakazi pamoja na Bodi. > Kujaribu kupunguza ushiriki wa mashirika ya kijamii hakutafanikiwa na > kunaonyesha upotovu huu wa hali ya juu. ICANN inahitajika kuwa na > nyakati za maoni ya umma kwa maana ni lazima isikize na kujibu > maswala ya jamii. Maoni ya umma hutokana na kuwepo kwa mawasiliano > na mazungumzo kuhusu hata maswala tata, hata kama ni miito ya > kuchukua hatua. Hakuna mpango au sheria inayoipa ICANN au > wafanyakazi wake uwezo wa kuamua kutotilia maanani au kupuuza > vikundi karibu vyote vilivyoonyesha kutaka kushiriki kwenye > marekebisho > ya GNSO, eti kwa sababu wamewashutumu wafanyakazi wa ICANN. > > Jaribio la ICANN la kutaja maoni haya ya muhimu kama “kampeni ya > uandikaji barua” inapuuza ushiriki wa siku zijazo na imani katika > mipango ya ICANN ya kuhusisha umma. > > Porojo ya Nne > > "Mashirika ya kijamii yamegawanyika kuhusu swala la katiba ya NCSG." > > Si Kweli. Hakujawahi kuwa na maoni ya umma yaliyoegemea upande mmoja > kama haya katika historia ya ICANN. Hata kama wafanyikazi wa ICANN > wanaiambia Bodi kwamba mashirika ya kijamii yamegawanyika, maoni zaidi > yanakataa katiba iliyopendekezwa na ICANN na kuiunga mkono > iliyopendekezwa na NCUC. Wanabodi wanaotegemea habari kutoka kwa > wafanyikazi wa ICANN pekee wanaweza kuamini kwamba mashirika ya > kijamii yamegawanyika , lakini wanabodi ambao wanesoma maoni ya umma > wanaweza kuona umoja wa mashirika ya kijamii katika kupinga > kulazimishwa > kufanya ICANN inavyotaka. > > Porojo ya Tano > > "Mashirika ya Kijamii yaliyoko kwa sasa hayawakilishi kamili > washikadau wote" > > Si kweli kwa vyovyote. Kwa sasa, kikundi cha mashirika ya kijamii, > kijulikanacho > kama NCUC kina wanachama 143 ambao kati yao 73 ni mashirika yasiyo ya > kibiashara na watu banafsi 70 kutoka nchi 48. Hili ni ongezeko la > 215% tangu > kanuni ya uakilishaji wa wote ianzishwe. > > Ushiriki wa jamii isiyo ya kibiashara umeongezeka na kwa hivyo si > haki kusema > kusema kwamba NCUC haishirikishi washika dau wote bila ya kusema > hivyo juu > ya jamii zingine. Hata mwaka wa 2006, utafiti huru uliofanywa na > London School > of Economics ulionyesha kuwa NCUC iliwakilisha maeneo mengi zaidi > na pia > ilikuwa na watu wengi zaidi tofauti katika kamati ya GNSO wakati > wowote, na > kwamba ilibadilisha zaidi wawakilishi wake katika kamati hio > ikilinganishwa na > jamii zile zingine sita. > > Kwa upande mwingine, jamii ya wanabiashara imekuwa ikiwakilishwa na > watu > wale wale 5 kwa Kamati kwa muongo mmoja na kulipokuwa na mwito wa > marekebisho ya GNSO, 3 kati ya wanakamati 6 wa jamii ya kibiashra > watawakilisha Marekani. > > Porojo ya Sita > > “ALAC inapendelea mkataba uliopendekezwa na wafanyakazi wa ICANN > kuliko ule wa mashirika ya kijamii” > > Uwongo: Kiongozi mmoja wa ALAC alisema kuwa anapendelea maktaba > uliopendekezwa na wafanyikazi. Wafanyikazi walichukua msemo huo na > kuupeleka kwa Bodi ya ICANN huku wakidai kwamba ALAC inapendelea > mkataba uliopendekezwa na wafanyikazi wa ICANN. Kwa kweli, taarifa > rasmi iliyotolewa na ALAC na iliyopitishwa na na ALAC ilisema kuwa > wanachama wengi wa ALAC waliunga mkono pendekezo la “kulitenganisha > swala la viti vya Kamati kutoka kwa maeneo ni jambo nzuri na mwelekeo > mwema.” > > Porojo ya Saba > > "Mkataba wa NCUC utakipa kikundi kile kile kidogo viti 6 badala ya 3" > > Uwongo: Kwa miezi minane iliyopita, NCUC imekuwa ikitangaza kuwa > itajitawanya muda tu NCSG itakapoundwa. Haina maana kuwa na “jamii ya > mashirika yasiyo ya kibiashara” na vile vile “washika dau wasio wa > kibiashara” kwani haya ni maneno yenye maana sawa. Kwa hivyo, viongozi > wa NCUC hawatakuwa na uwezo wa kuendesha NCSG mpya – uongozi mpya > utachaguliwa. Chini ya mkataba, mashirika na watu wote binafsi > watapiga > kura kuchaga viti vya Kamati, na si tu wanachama wa hapo mbeleni wa > NCUC. Masharti makali kuhusu uakilishi kutoka maeneo yote ya > kijografia > yatamaanisha kuwa wanaowania kutoka maeneo yote duniani > watachaguliwa hata kama hawatapata wingi wa kura. > > Porojo ya Nane > > "NCUC haitagawana viti vya Kamati na jamii zingine za mashirika yasiyo > ya kibiashara." > > Si Kweli: Mkataba wa NCUC uliundwa ili kuwezesha mashirika yasiyo ya > kibiashara kuwa na wawaniaji wao wa viti vya Kamati. Ikilinganishwa na > uwepo na uanachama wa NCUC, jamii nyingi zenye ajenda zinazoshindana > zitajitokeza. Kukua kwa maeneo kutoka mashinani hadi juu ni bora > kuliko mwelekeo wa Bodi/Wafanyikazi- pia unafanana zaidi na mapedekezo > ya BGC. Maktaba wa SIC unaelekeza uundaji wa maeneo kutoka juu na hii > ni ngumu na inaipa Bodi uwezo uliozidi kuamua “ushirikishaji” au > “umuhimu” wa washiriki wapya. Kwa vile uakilishi wa maeneo unategemea > viti vya Kamati. Viti vya Kamati vikilinganishwa na maeneo, kila eneo > litakuwa na mivurutano kuhusu kupewa kwa viti hivi vya Kamati > > Porojo ya Tisa > > "NCUC inataka kunyakua haki ya Bodi ya kupitisha maeneo” > > Uwongo: Watu wanaosema hivi ni dhahiri ya kwamba hawajasoma mkataba > uliopendekezwa na NCUC. NCUC inapendekeza kwambo Bodi iwe na uwezo wa > kupitisha au kukataza maeneo mapya yaliyoundwa chini ya mkataba huo. > > Pendekezo letu ni kuwe na na mielekezo ya kufuatwa (k.m nambari ya > wagombea) kwa kuundwa kwa maeneo mapya halafu mapendekezo > yatumwe kwa Bodi. Dhana ilikuwa kupunguza mzigo wa uundaji wa > maeneo mapya kwa > wagombea na pia kwa Bodi. > > Mkataba uliopendekezwa na NCUC una mapendekezo rahisi sana ya kuunda > maeneo mapya ukilinganishwa na ule wa SIC ambao utafanya uundaji wa > maeneo mapya kuwa jambo gumu sana. > > Porojo ya Kumi > > “Azma ya kuwa na eneo ni kuwa na kiti kwenya Kamati ya GNSO.” > > Uwongo: wengine hudai kwamba viti vya Kamati ya GNSO lazima > vilinganishwe kikamili na maeneo haswa kwa vile eneo halina maana bila > kuhakikishiwa kiti kwenye Kamati ya GNSO. Lakini, kusema hivyo ni > kutoelewa umuhimu wa maeneo katika GNSO mpya, ambao ni kuwapa sauti na > namna ya kushiriki katika utengenezaji wa sera –wala si kuhakikishiwa > kuwa na mjumbe asiye hata na mori wa kuafikiana na maeneo mengine. > > Viwili kati ya vikundi vitatu vya washikadau (Registries and > Registrars) > vilipitisha mwelekeo wa mkataba wa NCUC wa kutenganisha > viti vya GNSO kutoka kwa maeneo, walakini NCUC imekatazwa kuchagua > wajumbe wake kulingana na SG. > > Ungana na NCUC > > Mashirika na watu wote binafsi kutoka jamii ya wasio wanabiashara > wanaalikwa kuungana na NCUC kwenye mpango ya utengenezaji wa sera za > GNSO ya ICANN. Leta maoni yako kwa mazungumzo ya sera za mtandao wa > Internet na usaidie kulinda watumizi wa mtandao wasio wa kibiashara > kwa kushiriki kwa ICANN kupitia kwa NCUC. Ingia leo kwa kwenda hapa: > > http://icann-ncuc.ning.com/main/authorization/signUp? > ---ends---- > > About Grace: > ===================================================== > Grace Mutung’u (Bomu) is a young Kenyan lawyer who has been part of > the Kenya ICT policy process since 2005. She works with theatre > companies as an actor, marketer and cultural policy advocate. She is > currently taking a course Intellectual Property Law and the Internet > at Diplo Online Campus. > > Grace is a member of the ICT Consumers Association of Kenya. > ====================================================<grace > mutungu.jpg> IP JUSTICE Robin Gross, Executive Director 1192 Haight Street, San Francisco, CA 94117 USA p: +1-415-553-6261 f: +1-415-462-6451 w: http://www.ipjustice.org e: [log in to unmask]